Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, January 08, 2010

Picha ya kukumbukwa; Raisi Jakaya kikwete alipokuwa akizitembelea nyumba za wapigakura wake wa ki- Wahadzabe Mwaka mmoja na nusu uliopita. Kabila hilo linaishi msituni huku wakitegemea chakula kinachotokana na matunda ya porini pamoja na mizizi,
Rais aliagiza wanafunzi wa Kihadzabe ambao wanamaliza shule ya msingi wakifaulu, wapelekwe katika shule za sehemu nyingine ili waweze kuchanganyika na watu wengine.
“Hawa tukiwaacha waendelee kusoma wao peke yao hawawezi kujua kama kuna watu wengine humu duniani…mimi wakati nasoma pale Msoga kisha nikapelekwa Lugoba nilikuwa najua dunia hii ni ya Wakwere tu, lakini nilipoenda Kibaha Sekondari nikaona kumbe pia kuna watu wa kabila nyingine.Alisema JK...Picha na Maelezo

0 comments: