Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, March 04, 2010

Mfululizo wa majanga ya asili; Haiti, Chile, Uganda, Mexico, Msumbiji , na Kilosa Tanzania. tukio la karibuni kabisa ni la Uganda. Eneo la ramani lililo na alama nyekundu. Mvua imenyesha ghafla mapande ya ardhi yanamegeka na kuelekea bondeni. Hebu fikiria hali ilivyokuwa ngumu. Unaweza kujionea kwa kuchungulia taarifa ya TV ya Aljazeera hapo chini

Unaweza kuona hali ilivyokuwa mara baada ya kuporomoka kwa udongo kutoka mlima Elgon



Uganda ilikuwa hali ya kutisha , shule ya msingi imefunikwa ikiwa na watoto na zahanati pamoja na mashamba. Hadi sasa watu 300 wanaaminika kufariki.

Huko Chile nako tetemeko watu wamepoteza maisha...
Victoria Hermandez mbele ya nyumba yao huko Dichato, chile ambako tetemeko la ardhi lilitokea siku ya jumamosi nchini humo. bado wazazi wake wako chini ya vifusi na aaamini kuwa bado wao hai.

0 comments: