Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, March 01, 2010

Museveni na mkewe Janet na mtoto wao Lt. Col. Kainerugaba.


Chama Kikuu cha Upinzani nchini Uganda kinamtuhumu Raisi Yoweri kaguta Museveni kwa kumuandaa mtoto wake kuchukua nafasi yake pindi akistaafu. Mwanawe huyo Lt Col Kainerugaba Muhoozi, kwa sasa ni mkuu wa kikosi maalum cha kumlinda Raisi Museveni Hussein Kyanjo kiongozi wa Chama cha upinzani amenukuliwa akisema kuwa "Dhahiri anauandaa mwanawe ili kuendeleza utawala wa kifalme ." Maneno hayo yanaweza kuaminika kwani tayari mkewe Janet Museveni ni mmoja wa mawaziri wake anayehusika na eneo la Karamoja.Kaka yake mkubwa Museveni Generali Caleb Akandwanaho ni mshauri mwandamizi wa masuala ya ulinzi nchini humo wakati shemejiye Sam Kutesa ni waziri wa mambo ya Nje- . Kama hiyo haitoshi binti yake Natasha Karugire ni katibu muhtasi binafsi wa Raisi na ndugu mwingine wa mkewe Hope Nyakairu amemuingiza Ikulu akishughulikia masuala ya fedha.
Msemaji wa Jeshi la nchi hiyo Felix Kulaigye amenukuliwa akisema kuwa mtoto huyo wa Raisi mwenye miaka 36 Muhoozi hajafanya kosa lolote la kijinai hivyo ana uhuru wa Kugombe uraisi akipenda.

0 comments: