Madaktari nchini India wanaumiza vichwa wakimfanyia uchunguzi babu wa miaka 83 ambaye anadai hajakula wala kunywa maji kwa zaidi ya miaka 70. Tangia wameanza kumfanyia uchunguzi babu huyo siku nane zilizopita babu huyo hajakula, hajanywa kitu chochote na wala hajaenda chooni.
Madaktari wa jeshi la India wanamfanyia uchunguzi babu mwenye umri wa miaka 83 ambaye inadaiwa hajakula wala kunywa kinywaji chochote kwa zaidi ya miaka 70.
Wanajeshi wanaamini kuwa wakigundua siri inayomfanya babu huyo awe hali wala kunywa chochote, wataweza kuwapa njia wanajeshi kukaa muda mrefu bila kula wala kunywa.
Babu huyo mwenye nywele ndefu na ndevu ndefu aliyejulikana kwa jina moja tu la Jani, amekuwa akifanyiwa uchunguzi masaa 24 na timu ya madaktari 30 katika hospitali ya mji wa Ahmedabad magharibi mwa India.Jani anafanyiwa uchunguzi kwa wiki tatu kuthibitsha kuwa hali wala kunywa kitu chochote na tangia uchunguzi huo ulipoanza aprili 22 mwaka huu babu huyo hajakula, hajanywa kitu chochote na wala hajaenda haja ndogo wala kubwa.Video kamera mbili zimewekwa kwenye chumba chake zikifuatilia miendendo yake yote huku kamera moja imekuwa ikimfuatilia kila anapoenda kwa masaa 24."Matokeo ya uchunguzi wa mwili wake yatatupa mwanga jinsi binadamu wanavyoweza kuishi bila chakula wala maji", alisema Dr G. Ilavazahagan, anayeongoza uchunguzi wa babu huyo."Hii itatusaidia kuvumbua njia za kuwasaidia watu kuishi muda mrefu bila kula wa kunywa wakati wa majanga makubwa ya asili kama vile matetemeko ya ardhi".
"Dhumuni la kumfanyia uchunguzi Jani ni kujua anawezaje kuzihifadhi energy zinazohitajika na mwili wake", alisema Dr Ilavazahagan.
Jani ambaye huvaa nguo nyekundu akiwa na hereni kwenye pua yake ameishi maisha yake yote kwanye kijiji cha Charod kwenye jimbo la Gujarat.Jani anaelezea siri yake ya kuishi miaka mingi bila kula wala kunywa ni baraka alizobarikiwa na miungu ya kihindi tangia alipokuwa ana miaka minne.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, April 30, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment