Erico ni binti wa kijapani anayemudu kucheza kifaa cha Muziki wa kiasili wa Kabila la Wajaluo -Afrika Mashariki. anaongea na kuimba kwa Kijaluo. Leo alikuja katika studio za NHK kurekodi vipindi kama sehemu ya tamasha la maadhimisho ya 75 tangu matangazo ya NHK World kwenda hewani kabla ya kuwepo kwa Idhaa ya Kiswahili. Tumempenda kwa jinsi anavyotupenda Waafrika na mila zetu na jitihada zake za kuitangaza Afrika nchini Japani.Arigato Gozaimashita!
Anyango akiwa katika tumbuizo la wazi katika studio za NHK leo.
Tupo na Bi. Anyango , msichana wa Kijapani anayemudu vyema kucheza chombo cha Nyatiti cha kabila la wajaluo kule Kenya na anaongea kijaluo na Kiswahili kwa ufasaha...take five Anyango!...anadumisha mila yetu..
Tupo hapo mie na mwenzangu Edward Kadilo na wachezaji wa bendi ya Warembo ya Anyango , muda mfupi baada ya onyesho lao...
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Monday, May 03, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Kwa ndugu zangu hapa Tanzania wanaoibeza lugha ya Kiswahili na kuzitukuza za kigeni wanapaswa kujifunza kutoka kwa huyu binti wa Kijapani kuwa wewe ukisema cha nini mwenzio anasema nitakipata lini?
"JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI"
R.Njau
Mdau na mtetezi wa Kiswahili
Dar es salaam.
Post a Comment