Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, May 25, 2010

Katibu Mkuu Msaidizi wa jumuia ya watanzania wanaoishi nchini Japani Tanzanite Bw. Abby Senkoro(Pichani) ametoa taarifa inayowakumbusha wanachama wa jumuia hiyo kuwa tafrija ya kumuaga ofisa ubalozi Bw. Maleko na kumkaribisha Mh. Balozi Mama Salome Sijaona, Balozi mpya wa TZ hapa JP. Bw. Senkoro Kushoto na Kulia Bw. Prosper...


Hafla hiyo itafanyika siku ya Jumapili tarehe: 30/05/2010 huko Yamatoshi-Kinroufukushi-Kaikan Ni dakika 5 kutoka Tsuruma Station)na nikuanzia saa 10 jioni mpaka saa 2 usiku.
Bw. Sankoro amesema kuwa uongozi unawaomba wale wote waliojiandikisha kufika siku hiyo kufika kwa muda unaotakiwa ili tuweze kumaliza shughuli kwa muda tunaotakiwa. Na kwa wale waliojiandikisha na kupatwa na dharura tafadhali tunawaomba kutoa taarifa kwa viongozi walioandikisha majina yao haraka iwezekanavyo.
Amesema kuwa wale ambao hawajajiandikisha hawataruhusiawa kuingia ukumbini. Hivyo basi wale wote ambao hawajafanya zoezi hilo wanaombwa wafanye hivyo mpaka kufika tarehe 26/05/2010.
Maelezo ya jinsi ya ukumbini : Kutokea Shinjuku inachukua takriban saa moja kwa treni ya haraka (Odakyu line). Badirisha treni ukifika Sagamioni station upande wa Katase Inoshima line na ushuke Tsuruma station. Ukumbi uko dakika 5 toka kituo cha treni.Angalia Ramani


Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani Bw. Elibariki maleko (Pichani) anayetarajiwa kuagwa siku hiyo baada ya Kumaliza kipindi chake cha Utumishi hapa nchini pamoja na kumkaribisha Balozi mpya wa Tanzania hapa nchini Mh. Salome Sijaona.

1 comments:

Anonymous said...

Ni furaha sana kwangu na kwa familia yangu hapa Dar es salaam kuungana nanyi huko Tokyo katika tafrija ya kuagana na kakangu na mlezi wangu mpendwa sana ndugu Elibariki Maleko.Katika lugha yetu ya Kiswahili hakuna fungu la maneno wala sentensi ya kuonyesha hisia za shukrani kutoka katika papachi za moyo zaidi ya kusema asante.Nami nasema:ASANTENI KWA UKARIMU WENU KWA KAKANGU.
---------------------------------
R.Njau
Dar es salaam