Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, June 06, 2010

Familia ya mmoja wa wake wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imelazimika kumlipa Zuma fidia ya mbuzi mmoja mweupe kama kumuangukia Mkuu huyo wa nchi baada ya kugundulika kuwa mke wake Nompumelelo Ntuli (pichani akiwa na Raisi Zuma hivi karibuni huko India)huyo wa rais Zuma aliisaliti ndoa yake na kula uroda na mlinzi wake.


Imebainika kuwa Mke huyo Nompumelelo Ntuli alifukuzwa toka nyumbani kwa Zuma siku chache kabla ya krismasi mwaka jana baada ya kugundulika alimsaliti Zuma na kutembea nje ya ndoa.Ntuli alimpa uroda mlinzi wake, Phinda Thomo mkazi wa Dobsonville, Soweto. Mlinzi huyo alijiua mwenyewe baada ya siri kufichuka kuwa ametembea na mke wa rais, na alijua kuwa yatampata makubwa ...bora atangulie!
Bi. Ntuli ambaye hivi sasa yuko pamoja na Zuma katika safari ya kiserikali nchini India, ana mimba ya mtoto anayetarajiwa kuwa mtoto wa 21 wa Zuma. Hata hivyo maswali mengi yamezuka kuhusiana na ukweli wa baba wa mtoto huyo aliye tumboni mwake.
Taarifa zinasema kuwa Ntuli mwenye umri wa miaka 35 aliamua kufanya hivyo baada ya kukasirishwa na hatua ya Zuma kutangaza kuoa mke wa tatu.Taarifa zaidi zinasema kwamba Ntuli alimtukana mke wa tatu wa Zuma Tobeka Madiba na pia alitishia kutohudhuria harusi yake iliyofanyika mwezi januari mwaka huu, hata hivyo alibadilisha uamuzi wake na kuhudhuria harusi hiyo lakini alifukuzwa na kurudishwa kwao wakati wa sherehe za kitamaduni za harusi hiyo.Ntuli alisindikizwa na wazee wa kijadi hadi kwenye nyumba ya familia yake ambapo alikabidhiwa kwa wazazi wake.
Ntuli aliambiwa kuwa kitendo chake cha kuisaliti ndoa yake kimeikasirisha familia ya Zuma na mizimu ya mababu.Ili kuweka mambo sawa mwezi aprili mwaka huu, familia ya Ntuli ilienda kwa mzee Zuma na kumlipa fidia ya mbuzi mmoja mweupe ambaye alichinjwa siku hiyo hiyo.Habari za Ntuli kumsaliti Zuma zimeigawanya Afrika Kusini ambapo watu wengi wanampongeza Ntuli wakisema kuwa kama Zuma anazisaliti ndoa zake kwanini wake zake nao wasimsaliti.
Mmoja wa watu waliopiga simu redioni kujadili suala hilo alisema kuwa Zuma ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 68 hayawezi tena mambo ndio maana mke wake ametembea nje.Sijui bwana! Picha hapo chini inaonyesha list kamili ya wake wa mh. Jacob Zuma .

Kutoka Kushoto; Nompumelelo Ntuli, Thobeka Madiba, Mh. Jacob Zuma, na Mke Mkubwa kulia kabisa Sizakele Makhumalo. (Habari na Nifahamishe)

0 comments: