Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, June 27, 2010

Huko RUSTENBURG, Afrika kusini;Mchezaji Asamoh Gyan alfajiri ya leo aliwatoa kimasomaso waafrika baada ya kufunga goli la ushindi dakika ya tatu katika muda wa ziada dhidi ya timu ya Marekani katika mzunguko wa pili wa mtoano kombe la dunia huko Afrika Kusini.

Timu hiyo sasa inatinga robo fainali ikiwa ni timu ya tatu ya kiafrika kupata kuingia katika hatua hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya moja kwa moja katika dakika 90 za awali na sasa Ghana itakwaana na Urugway siku ya ijumaa katika jiji la Soccer city katika robo fainali.
Katika mechi hiyo Marekani iliwakilishwa na Tim Howard, Steve Cherundolo, Carlos Bocanegra, Jay DeMerit, Jonathan Bornstein, Landon Donovan, Michael Bradley, Ricardo Clark (Maurice Edu, 31), Clint Dempsey, Jozy Altidore (Herculez Gomez, 90), Robbie Findley (Benny Feilhaber, 46).
Huku Ghana ikiwa na ;Richard Kingson, Hans Sarpei (Lee Addy, 73), Asamoah Gyan, John Pantsil, John Mensah, Anthony Annan, Samuel Inkoom (Sulley Muntari, 113), Jonathan Mensah, Dede Ayew, Kwadwo Asamoah, Kevin-Prince Boateng na kocha (Stephen Appiah, 78).


Full mapambo usoni....
Mdada wa Afrika Kusini akifurahia pilikapilika za Kombe la Dunia.

0 comments: