Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, November 02, 2010


Mgombea wa CCM nafasi ya uraisi wa Zanzibar Dr. Mohamed shein ameibuka kidedea baada ya kushinda uchaguzi huko visiwani kwa asilimia 50.1. na Maalim Seif asilimia 49.1.


Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatibu Mwinchande akitangaza matokeo...

Mpinzani wake mkubwa Maalim Seif Hamadi ametoa hotuba ya kukubali matokeo hayo .Na kusema kuwa kulikuwa na dosari lakini safari hii hakuna mshindi , isipokuwa wazanzibari wote wameshinda....

Maalim Seif akitoa hotuba ya kukubali matokeo...hotuba hiyo ilikuwa ikitangazwa live na TBC na kuonekana duniani kwa njia ya mtandao.
Kulikuwa na hali ya taharuki katika hoteli ya Bwawani ambako shughuli ya kutangaza matokeo ilikuwa ikifanyika , pale wafuasi wa CUF walipokuwa wakidai kuchelewa kutangazwa matokeo ilikuwa njama.

Wafuasi wa CUF Bwawani ....
Lakini Maalim Seif aliwataka wawe wastahimilivu ili kutovunja amani na kuviingiza visiwa hivyo kwenye mtafaruku.

0 comments: