Hii ina nikumbusha Ivory coast. Mungu apishilie mbali yasitokee kama ya Kenya .
Huko Ivory Coast tunaelezwa kuwa ...Tayari Raisi wa zamani wa Afrika Kusini na mwakilisi wa AU Thabo Mbeki, amekwishakutana na wagombea wawili wa rais wa Ivory Coast ambao walijitangaza kuwa rais wa nchi hiyo mjini Abidjan hapo siku ya Jumapili ilikutafuta suluhisho la mgogoro huo.Bw. Mbeki aliwambia waandishi habari kwamba amekwenda huko kusikiliza kila upande ili kufahamu jinisi hali ilivyo lakini Bw. Outtara amewambia waandishi habari kwamba alimuarifu Bw. beki kwamba yeye ndiye rais wa halali wa nchi na amemtaka Bw. Gbagbo kumkabidhi madaraka.
Laurent Gbagbo alikula kiapo ya kuiongoza nchi siku ya Jumamosi kwa misingi kuwa, baraza la katiba limempa ushindi wa asilimia 51 ya kura. Takriban asilimia kumi ya kura zilibatilishwa kwasababu ya ubadhirifu.
Madai ya Bw. Ouattara ya kushinda uchaguzi yanaungwa mkono na Jumuia ya Kimataifa.
Hakuna dalili ya kumalizika kwa mzozo huu kwa urahisi labda kwa kugawana madaraka , fomula iliyo nyepesi pindi maamuzi ndani ya masanduku ya kura yanapochafuliwa .
DKT. NCHEMBA AKARIBISHA SAUDI ARABIA KUWEKEZA TANZANIA
20 minutes ago
0 comments:
Post a Comment