Wagombea wote wa nafasi ya Uraisi nchini Ivory Coast ambao walipambana katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini humo wameamua kujiapisha kila mtu kivyake na hivyo kuwa na nchi yenye 'Maraisi wawili' wakati huu , hali inayolikaribisha taifa hilo kwenye vita na machafuko makubwa.
Rais anayetetea kiti chake Laurent Gbagbo(anayeapa hapo chini) alikuwa wa kwanza kujiapisha na saa chache baadaye mwenzake naye Alassane Ouattara pia akala kiapo kuliongoza taifa hilo kwa uaminifu mkubwa na kwa maana hiyo kuwa nchi ya kwanza duniani katika historia kuwa na maraisi wawali na kwa maana hiyo Maamiri majeshi wakuu wawili...imagine!.
Marekani, Umoja wa Mataifa na Ufaransa zimesema Bw Ouattara ndiye ameshinda uchaguzi huo.Bw Ouattara alitangazwa mshindi la Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo yalitenguliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.
Uchaguzi wa raundi ya pili ya urais, ulikuwa na lengo la kuliunganisha taifa hilo ambalo ndio mzalishaji mkubwa zaidi ya kakao duniani, baada ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
Maelfu ya wakazi wa nchi hiyo waliingia mitaani kwa maandamano wakipinga hatua ya Bw Gbagbo, wakisema hayo ni mapinduzi. Huku wafuasi wa Gbagbo wakiangusha kicheko kilichojaa wasiwasi. Inavyooelekea Allassane Ouattara anaungwa mkono na watu wengi nchini humo kuliko mwenzake...unaweza kuangalia sehemu ya kampeni zake...
Wafuasi hao wa Bw Gbagbo wanasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa hauna haki ya kusema nani ni mshindi, na wametishia kuwafukuza wafanyakazi wapataoo 8,000 wa umoja huo. Sijui ! lakini sakata hili haliwezi kwisha hvi hivi bila ghasia na pengine vifo...
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, December 05, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment