Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, January 16, 2011


Habari za punde kutoka Johannesburg nchini Afrika kusini zinadokeza kuwa , uvumi umezagaa jijini humo kuwa Raisi wa zamani wa nchi hiyo Mzee Nelson Mandela yu taabani anaumwa na hali yake ni majaaliwa.


Msemaji wa mfuko wa Nelson Mandela Sello Hatang alkanusha taarifa hizo jana jumamosi na kusema Mzee Mandela mwenye miaka 92 alikuwa katika mapumziko na mkewe Graca Machel na kwamba walikokwenda na wanachokifanya ni siri yao wawili na ni haki ya faragha.
Hata hivyo kuna habari kuwa hali ya mzee huyo imezorota mno na wengine wamekuwa wakiwasiliana wakisema kuwa amekufa ja,bo ambalo limekanushwa vikali na watu wake wa karibu.Hata hiyo vyanzo vya uhakika vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimeonyesha kuanza kukubaliana na uvumi huo.
Source: www.news24.com/SouthAfrica

0 comments: