Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, January 13, 2011

Mieleka ya sumo ni mchezo maarufu nchini Japani ulioanza miaka kwa maelfu .

Mchezo huu sio tu ulianza kama njia ya kuonyesha ushujaa lakini pia ulihusiana na imani za kidini na zamani (Miaka elfu kadhaa ) ulichezwa pia katika madhabahu ya kishinto huko Ugiriki, Babylon, Misri ,Sumaria, na nchini India na mnamo mwaka 776 BC ulifanya kama njia ya kushindanisha wababe.


Mchezo unaotumia nguvu nyingi baina ya watu wawili wanaofahamika kwa kijapani kama rikishi , na mshindi anapimwa kwa kumtoa mpinzani wake nje ya ulingo ‘dohyo’ ama kumuangusha chini . Mchezo huu ulianzia Japani na hadi sasa ni nchi pekee inayoendesha ligi ya kulipwa ya mchezo huu .Mchezo huu unahusishwa na masuala ya kitamaduni ya ukale yanayoonyesha ushuja na unahusiana pia na imani za kidini za hapa Japani nah ii inajitokeza pale chumvi inapotumika kama moja ya kitendea kazi wakati wa mashindano ambapo wanamieleka huimwaga kila kona ya jukwaa lao kuondoa mikosi.
Kama ilivyo kwa michezo mingine , wachezaji wa sumo wa kulipwa hapa Japani wamewekwa katika madaraja kadhaa unaweza kuangalia huo mchoro . Daraja la chini kabisa ni Jonokuchi na la juu ndio hilo Yokozuna.

0 comments: