Polisi wa kutuliza ghasia nchini Bahrain wamewatawanya waandamanaji kati uwanja maarufu ulio katikati ya nchi hiyo na hivyo kuwalazimisha kurejea eneo ambalo awali walikuwa
.Walifika hapo wakakutana na polisi na baada ya nusu saa hivi Polisi wakawamwagia risasi na kuwauwa waandamanaji kadhaa hapo hapo kama unavyoweza kuona kwenye video hiyo ilichukuliwa na mwandishi wa habari wa Shirika la Aljazeera la Qatar.
Waandamanaji hao walikuwa wakipiga mayowe huku wakiibusu ardhi huku wakichukua picha na magari ya polisi yanayokadiriwa kufikia 60 yakliwazunguka.Hospitali maarufu ya Salmaniya imekuwa ikipokea majerhi na maiti za waandamanaji.Inasemekana kulikuwa na maagizo ya familia ya kifalme inayoongozwa na mfalme mwenyewe Hamadi bin Issa bi Khalifa kuhakikisha mitaani hakuna watu na Polisi walitekeleza amri hiyo bila kujali maisha ya watu.
Mamia wa akinamama waliovaa abayas nyeusi ( Baibui na hijabu) waliungana katika maandamano hayo yanayoitaka Serikali ya kifalme kuondoka na kuingia ya kidemokrasia.
Wasiwasi umetanda nchini humo , na kipandauso hicho kimezaa kwa viongozi wote katika nchi za kiarabu... (Taarifa na Aljazeera)
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, February 20, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment