Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, February 27, 2011

Mahakama moja katika Mkoa wa Saitama hapa Japani imewahukumu wanaume wawili miaka miwili jela kila mmoja kwa kushindwa kumkataza rafiki yao aliyekuwa amekunywa pombe wakiwa pamoja naye kuacha kuendesha gari , hali ambayo ilisababisha kupata ajali barabarani.


Tukio hilo ni la mwaka 2008 lakini hukumu imetolewa juzi huku wakili wao akisema kuwa ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kuwakumu watu kwa kushindwa ‘kutimiza wajibu wao wa kumkataza mtu aliyekunywa pombe kuacha kuendesha gari.
Uamuzi huo wa kuwafunga watu hao umefikiwa na jopo la majaji wazoefu na majaji watatu wa kiraia (Kama wazee wa baraza kule Tanzania) . Jaji aliyeongoza jopo hilo Makoto Tamura amesema kuwa anamuadhibu Isao Oshima mwenye umri wa miaka 48, na Junichi Sekiguchi (46) kwa kumruhusu mwenzao kushika usukani bada ya kunywa pombe.

Katika siku hiyo , gari la watu hao liligongana na jingine lililokuwa likija mbele yao huko Kumagaya mkoa wa Saitama na kuwaua wapenzi wawili . Dereva mwenyewe alihukumiwa kwenda jela miaka 16.

Timu ya mawakili inayotoa utetezi imesema kuwa haijafurahishwa na hukumu hiyo na familia hiyo inataka kukata rufaa.
(Tafadhali..picha hizo hazina uhusiano wa moja kwa moja na habari hii ni mfano wake)

0 comments: