Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, March 08, 2011

MCHUNGAJI Amilikine Mwasapila anayeaminika kupewa dawa ya kuponya UKIMWI na Mwenyezi Mungu kwa njia ya ndoto amebainisha kuwa mgonjwa akinywa dawa hiyo ndani ya siku saba atakuwa amepona ugonjwa huo akaongeza kuwa hata kama Virusi vya Ukimwi vikiendelea kuonekana baada ya kufanyiwa vipimo Hospitali bado havitakuwa na nguvu ya kushambulia mwili wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Kijijini kwake Samunge wilayani Loliondo na sehemu ya habari kwenye blogi hii kuchotwa kutoka katika gazeti Mtanzania Mch. Amilikine alisema kuwa Mungu ndiye aliyemuotesha kwamba ameweka Neno lake la uponyaji ndani ya Mti.Ambapo maagizo ya Mungu katika ndoto hiyo yalikuwa ni kuuchimba, kuchemsha mti huo kisha kupatia mgonjwa kikombe kimoja kwa Sh 500 tu.

Hivi sasa barabara ya Mto wa Mbu kupitia Oldonyo Lengai kumekuwa na mafuriko ya watu wenye matatizo mbalimbali wanaoelekea katika kijiji cha Samunge kwa ajili ya kunywa kikombe kimoja cha dawa. Hongera mchungaji. Shukuran Mgosi Peter Omari wa Rock City...
Habari za mchungaji huyu zinasambaa kama moto wa nyasi kavu kote duniani...

0 comments: