MBUNGE mmoja nchini Kenya amefukuzwa nje ya bunge kwa kuvaa mavazi yasiyo na heshima.
Mbunge huyo wa jimbo la Makadara mjini Nairobi, Gidion Mbuvi, alifukuzwa kwenye kikao cha jana kwa kuvaa miwani ya jua na hereni ndogo za mawe yenye thamani.
Naibu spika wa bunge, Farah Maalim, alisema namna bwana Mbuvi alivyovaa haionyeshi heshima kwa bunge, ambalo halijawahi kuwa na mbunge mwanaume aliyevaa hereni na hivyo kumtaka atoke nje akavae vyema kabla hajarejea tena kwenye kiti chake. Na ndivyo ilivyofanyika. Hatahivyo, Naibu spika wa bunge alishutumiwa na wafuasi wa Mbuvi kwa kukosa uvumilivu. Ingawa kwa upande wake anaonekana kuzingatia kanuni za ueneshaji bunge kama alivyosoma hivyo vipengee mbele ya Bunge.
Mbuvi anajulikana kama Sonko, jina ambalo kwa lugha ya mtaani linamaanisha mtu tajiri anayeishi maisha ya kifahari.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, March 04, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment