Leo Alhamisi ilikuwa siku nzuri sana kwa wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Japani-NHK World ambapo walijumuika chini ya miti ya maua ya sakura iliyo katika Bustani ya Yoyogi karibu na jengo la utangazaji la NHK na kupata chakula cha mchana cha pamoja. Wafanyakazi wa Idhaa takriban 18 walikusanyika katika vikundi vikundi na kula vyakula vyao walivyotayarisha. Huu ni utamaduni wa wajapani ambapo katika wiki moja ya kila mwaka maua ya miti hii inapoanza kuchanua hukusanyika chini ya miti kula pamoja na kufurahi.
Nasi Idhaa ya kiswahili , tuliwakilisha na menyu yetu ilikuwa kali ugali na vitweleo vyake kadhaa (take five Bi> Anna na Bi. Specioza) , wakubwa walikula wakafurahi sana kama baadhi ya picha zinavyoonyesha.
Idhaa yetu ya Kiswahili iliwakilishwa na wadau Edward Kadilo, Jonas Songora , Anna Kwambaza na Bi. Specioza Mallya nami wa Mirindimo tukiongozwa na Mkuu wetu Kaori Note. Ilikuwa nzuri...kwahakika.
Maagizo ya rais ni nini?
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment