Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nchi za nje wa Ufaransa Alain Juppe amesema majadiliano ya kumshawishi kiongozi anayeng´ang´ania madaraka nchini Cote d´Voire kuondoka madarakani, yanakabiria kukamilika.Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa amewaambia wabunge wa nchi hiyo, kuwa anaamini kuondoka madarakani kwa Gbagbo kuko karibu.Maafisa wanasema kuwa kiongozi huyo amejificha kwenye handaki Ikulu jijini Abijan-pichani...na amependekeza masharti kadhaa juu ya kujisalimisha , baada ya mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi wanaomtii Alassane Ouattara,
Laurent Gbagbo anaendelea kung'ang'ania madaraka na wanajeshi wake wanaripotiwa kuwa wanakidhibiti kituo cha televisheni cha taifa. Laurent Gbagbo amewatolea wito wafuasi wake kuelekea barabarani na kupambana.Wakati huohuo,Marekani imemtaka Laurent Gbagbo kuachia madaraka haraka iwezekanavyo kwani anauhatarisha usalama katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.
DW
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, April 06, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment