Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, April 02, 2011

Mbwa mwenye 'bahati ya mtende' ambaye alisombwa na maji wki tatu zilizopita katika maafa ya mawimbi ya tsunami yaliyotikisa eneo la kaskazini Mashariki mwa japani ameokolewa akiwa hai ikiwa ni wiki tatu zimepita .
Mbwa huyo alikutwa na waokoaji wa ndege za kijeshi akiwa juu ya paa moja la nyumba juu ya vifusi katika Pwani ya mji wa Kesennuma, eneo la Miyagi. Baada ya majaribio kadhaa kukwama ya kumuokoa kutokana na mbwa huyo kuwakimbia waokoaji hatimaye walimfikia na kumuondoa hapo akiwa mnyonge ...alifunikwa mablanketi na kumkimbiza hospitali kuokoa maisha yake.

0 comments: