Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, May 12, 2011

Tukio la kushangaza na kusikitisha limetokea ndani ya Kanisa katika Parokia ya Vugu mkoani Kigoma, mwishoni mwa wiki iliyowaacha waumini na butwaa, baada ya Padri kumpiga makofi Bibi Kizee katikati ya ibada ya misa ya pili, akimtuhumu kuondoka na Sakramenti aliyoipokea madhabahuni.

Padri aliyefahamika kwa jina moja la Sabas, alifikia hatua hiyo wakati wa ibada ya Sakramenti, ambapo bibi huyo aliungana na waumini wengine kwenda kushiriki, lakini alipopewa kipande cha mkate, aliondoka nacho na kwenda kukila akiwa ameketi. Inaripotiwa kuwa kitendo hicho kilisababisha Padre Sabasi kusimamisha huduma hiyo ghafla, na kumfuata bibi huyo na kuanza kumpiga makofi.Waumini waliohudhuria ibada hiyo wameeleza kuwa ni mara ya kwanza kitendo hicho kutokea mkoani humo.
"Huyu ni mtu mzima, hivyo hakuweza kuvumilia kusimama na kukila kipande cha mkate na kuamua kukaa chini, Padri alitakiwa kumuonya kama alikuwa amekosea na siyo kumpiga, " alisema muumini mmoja mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo.Padri Sabas alipohojiwa kuhusu kitendo hicho alidai kuwa alifikia uamuzi huo kutokana na muunini huyo kwenda kinyume na utaratibu wa kanisa hilo na kuongeza kuwa, alimwona muumini huyo akikiweka kipande hicho kwenye ziwa (titi) kwa imani za kishirikina.
Bi. Kizee huyo aliondoka mara moja baada ya ibada hiyo.

0 comments: