Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, May 20, 2011

Maelfu ya wakazi wa dar es salaam leo walishiriki katika mazishi ya Shekhe Yahaya Hussein aliyefariki jana . Mazishi yalifanyika katika makaburi ya Tambaza .

Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa katika Makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Sheikh Yahaya Hussein alifariki dunia katika hospital ya Mount mkombozi iliyopo maeneo ya kinondoni.

Vyanzo mbalimbali vya habari vinasema kwamba Sheikh Yahaya alipelekwa hospitalini hapo ghafla leo asubuhi ktokana na tatizo la moyo na amefariki mnamo mida ya saa tano kasoro asubuhi ya leo.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu huyu peponi, Ameen.
Unaweza kuona kazi alizokuwa akizifanya wakati wa uhai wake kwa dakika kama saba hivi hapo chini:

0 comments: