Katika hatua inayoonekana wa rushwa inaogopewa nchini Japani kwa kiasi kikubwa ,Mwenyekiti wa Baraza la mji wa Kawasaki, mkoani Fukuoka amejiua juzi jumapili na kuacha kijikaratasi kikilaumu uchunguzi uliofanywa na Polisi kuhusiana na tuhuma za ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi unawahusisha wafuasi wake, kwamba kulikuwa na harufu ya rushwa .
Kulingana na taarifa za Polisi wa eneo hilo, Hidemi Morimoto mwenye miaka 67, dhahiri anaonekana amejiua mwenyewe kwa kuchoma mkaa fulani bandia katika gari lake katika jiji la Tagawa Fukuoka, akakosa hewa na kufa.Hidemi amekuwa akihojiwa na wachunguzi kuanzia siku ya Jumatano iliyopita hadi Ijumaa baada ya wafuasi wake wawili walikamatwa kwa tuhuma za kuwapa chakula wapiga kura kinyume cha sheria wakati wa kampeni za baraza la halmashauri ya Tagawa mwezi wa April.
Kulingana na familia yake , katika maandishi aliyoyaacha nyumbani kwake , Morimoto alikabiliwa na mahojiano makali na alilazimiswa kuwatambua watuhumiwa. Aliamua kujiua kabla ya kuhojiwa tena juzi Jumamosi. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo hapo nyumbani kwake…
Katika tukio jingine Mwili wa kijana mmoja wa kiume umepatikana chini ya jengo alilokuwa akiishi katika eneo la makazi ya watu huko Kobe juzi Jumapili. Polisi wanasema leo jumatatu kuwa kuwa kijana huyo anaonekana amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani. Mtu mmoja aliyepita katika eneo hilo aliwataarifu polisi jana Jumapili baada ya kuhisi kuna kijana mmoja amelala fofofo chini ya jengo la nyumba hiyo iliyopo eneo la Suma jana jumapili saa 11 alfajiri . Polisi walifika hapo na kuuchukua mwili wa kijana huyo hadi hospitalini na madaktari wakathibitisha kuwa alishafariki dunia.
Kijana huyo mwenye miaka 16 ambaye jina lake linahifadhiwa alikuwa anasoma katika shule ya sekondari ya juu ya gakuin hapo Kobe.Kulingana na maelezo ya Polisi , hakuna dalilizozote katika mwili wake zinazoonyesha kuwa alishikwa au kusukumwa na mtu yoyote na inakisiwa kuwa alijirusha kutoka ghorofa ya tano ya jengo alilokuwa akiishi na wala hajaacha ujumbe wowote.Ndugu wa kijana huyo waliokuwa wamelala wakati tukio hilo linatokea wamesema kuwa hawajui sababu yoyote iliyomsukuma kijana huyo kujiua na hakuna kilichobainika , shuleni wala nyumbani, polisi wamewaambia waandishi wa habari.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, May 31, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment