Maelfu ya watu wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa bingwa wa michezo ya Olimpiki mbio za marathon raia wa Kenya Sammy Wanjiru jana Jumamosi aliyefariki mwezi uliopita baada ya kuanguka kutoka kwenye ushoroba wa nyumba yake. Mazishi yalifanyika katika kijiji cha Heshima, eneo la Ol joroonok na kuongozwa na mjane wa Marehemu Trizah Njeri-pichani akiweka shada la maua.
Hata hivyo mama mzazi wa wanjiru alitinga nyumbani kwa Marehemu akiwa na panga alilolificha kwenye mfuko akidai kuwa atamkata nalo mtu yoyote anayeunga mkono mazishi hayo.
Hata hivyo mazishi yalifanyika katika uwanja wa michezo katika wilaya alikozaliwa, Nyahururu, katika jimbo la Rift Valley, huko Kenya chini ya ulinzi mkali wa polisi. Mahakama iliamuru wiki hii kuwa Wanjiru, aliyekuwa na umri wa miaka 24, anaweza kuzikwa licha ya kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo chake na kusema kuwa Wanjiru alikufa ama katika ajali, au alijiua baada ya mkewe kumfumania na mwanamke nwengine.
Mama yake Wanjiru, Hannah, alisusia mazishi hayo. Katika kile kinachoonyesha kupata heshima ya kitaifa alipigiwa saluti ya mizinga 21 wakati jeneza lake lilipoteremshwa kaburini katika shamba lake. Wanjiru alikuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za marathon za michezo ya Beijing mnamo mwaka 2008 na akihesabiwa kuwa mojawapo wa vijana chipukizi hodari.Mazishi yake yalihudhuriwa na wanariadha mashuhuri wa Kenya na watu mashuhuri.
Maagizo ya rais ni nini?
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment