Jana Ijumaa usiku katika Ubalozi wa Tanzania hapa Japani kulikuwa na hafla fupi iliyowakutanisha marafiki wa Afrika waliopo hapa Japani chini ya Shirika lao lisilo la kiserikali la 'Friendship International Center' ambalo huwahamasisha wajapani kulijua na kulipenda bara la Afrika. Wanachama wa Shirika hilo kutoka maeneo mbalimbali duniani walihudhuria hafla hiyo. Tanzani kupitia balozi wake Mh. Salome Sijaona na maafisa wa ubalozi huo waliitumia fursa hiyo kuinadi Tanzania vilivyo.
Baadhi ya vikorombwezo vya hafla hiyo ulikuwa Muziki wa kitamaduni za kijapani uliopigwa 'Live', video zilizoonyesha mandhali nzuri ya Tanzania na pia kulikuwa na mlo wa nyumbani , ambao ulionekana kuwakosha sana wajapani.Balozi Sijaona ndiye alikuwa mwenyeji wa ghafla hiyo. nasi tulikuwemo...unaweza kufuatilia tukio hilo kwa njia ya picha na video hapo chini...
Baadaye kulikuwa na utoaji wa zawadi kwa washindi waliojibu maswali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Tanzania...lilikuwa zoezi zuri sana ...sita kati yao waliibuka kidedea. Endelea kufuatilia tukio hilo kwa kutazama picha hapo chini...
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, June 04, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment