Mchezaji nyota wa Manchester United, Ryan Giggs amesababisha kuvunjika kwa ndoa ya kaka yake baada ya kugundulika alikuwa akimla uroda mke wa kaka yake kwa jumla ya miaka minane.
-Picha ;Ryan na nyingine akiwa na mkewe...Mchezaji mashuhuri wa Manchester United, Ryan Giggs ameingia kwenye kizaazaa kikubwa baada ya magazeti ya Uingereza kutoboa siri yake kuwa mbali ya kusailiti ndoa yake kwa kutembea na mrembo wa Big Brother, Imogen Thomas alikuwa pia akimla uroda mke wa kaka yake kwa miaka minane sasa.Imedaiwa kuwa Giggs alikuwa akijivinjari na mke wa kaka yake Rhodri Giggs kwa miaka minane na kuvuja kwa siri hiyo kumepelekea Rohdri kuamua kuivunja ndoa yake na mke wake.Rhodri mwenye umri wa miaka 34, alisema kuwa amehuzunishwa sana na habari za uhusiano wa kimapenzi kati ya Ryan Giggs na mkewe Natasha mwenye umri wa miaka 28. (Mrembo Imogen mwenye nguo nyeusi kwenye gari...)
"Nilikuwa na mke wangu Natasha siku ya jumamosi lakini kuanzia sasa siko naye tena", alisema Rhodri."Najua kwamba mimi na Ryan tulikuwa na migogoro wakati fulani lakini sikutegemea kama ingefikia hali hii ya kudhalilishana, nilihisi kuna kitu kinaendelea kati ya Ryan na Natasha lakini sikujua ni kitu gani", Rhodri.Gazeti la News of the World liliripoti jumapili kuwa Giggs alikuwa akilala na Natasha wakati mke wake alipokuwa mjamazito, na aliendelea kula uroda na Natasha siku moja baada ya mke wake kujifungua mtoto wa kike.Natasha inasemekana ndiye aliyeamua kuvujisha siri ya uhusiano wake na Giggs baada ya habari kuzagaa kwenye vyombo vya habari kuwa Giggs alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo aliyekuwa mshiriki wa Big Brother UK, Imogen Thomas.
"Nilipogundua kuwa alikuwa pia na uhusiano wa kimapenzi na Imogen, nilivunjika sana moyo", Natasha alitoboa siri kupitia kwa rafiki yake."Najua itaonekana ni jambo la kushangaza, mbali ya kumsaliti mkewe Stacey, alikuwa akinisaliti mimi pia kwa kutembea na Imogen", alisema mke huyo wa kaka yake Giggs.
Inasemekana Natasha na mumewe waiotalikiana walitoka siku za karibuni na kwenda kwenye mgahawa mmoja kwa chakula cha jioni na vijimaneno ndipo vilipoanza. Picha-Mgahawani-na Giggs mkubwa akiondoka nyumbani kwa huzuni akiwa amejifunika sweta asipigwe picha...Habari zaidi zimesema kuwa baada ya Natasha kuvihakikishia vyombo vya habari kuwa habari za uhusiano wake na Giggs kuwa ni za kweli, alisafiri pamoja na watoto wake wawili kwenda nje ya nchi.Rhodri kwa upande wake amebaki na majonzi nyumbani kwake ambapo inadaiwa kuwa marafiki zake wa karibu wanajaribu kumfariji kwa haya yaliyomkuta
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, June 08, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment