Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, July 07, 2011

Polisi nchini Japani imemfungulia mashitaka binti mmoja wa kijapani kwa kitendo chake cha kuongea na simu ya mkononi wakati akiendesha baiskeli. Hii ni kesi ya aina yake hapa nchini kutokana na ukweli kuwa japo kuna sheria inayokataza kitendo hicho lakini ni mara chache kesi hizo kujitokeza mahakamani. Saa tatu ya jumapili iliyopita , Polisi aliyekuwa akifanya doria huko Hiratsuka, katika mkoa wa Kanagawa , alimuona binti mmoja mwanafunzi wa sekondari mwenye miaka 15 akiwa anazungumza na simu akiwa anaendesha baiskeli na kwa maana hiyo kuvunja sheria ya barabarani na mbaya zaidi alipoambiwa aache kufanya hivyo alikaidi.
Mwanafunzi huyo alijikuta akiandikiwa hati ya kufikishwa mahakamani , ikiwa ni mara ya kwanza kwa polisi wa eneo hilo la kufikisha mahakamani shauri linalofanana na hilo , wakidai kuwa wanataka kukomesha vitendo vinavyofanywa na waendesha baiskeli hapa Japani vya kuongea na simu wakati wakiendesha baiskeli au kusikiliza muziki kwa kutumia vifaa vidogo vya muziki masikioni huku wakiwa katika mwendo mkali katika baiskeli zao.. Sheria inayokaza vitendo hivyo ilianza kutumika rasmi tarehe mosi mwezi Mei mwaka huu.Bila shaka binti huyo akipatikana na hatia atapigwa faini ya Yeni za kijapani elfu 50 sawa na fedha za kitanzania Takriban (Tsh. 975,000/=)
Nasi mashabiki wa baiskeli inabidi tuwe makini ...duh!-

0 comments: