Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, August 31, 2011

Wananchi wa Ludewa ambao ni wateja wa benki ya NMB tawi la Ludewa wametinga nyumba kwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wakitaka awasaidie kuishtaki benki hiyo kwa madai ya upotevu wa fedha zao katika mazingira tata.

Agnesi Mapunda ni mtumishi wa Halmashauri ya Ludewa idara ya ardhi ambaye ni mteja wa benki hiyo mwenye akanti namba 6012400590 NMB tawi la Ludewa ambaye alidai kuwa akaunti yake ilikuwa na fedha zaidi ya shilingi milioni 1 ila mwezi wa sita alikuta akaunti hiyo ikiwa na salio la shilingi 144,000 pekee na baada ya kuuliza aliambiwa fedha zake zimetolewa kwa huduma ya pesa fasta na NMB Mobel huduma ambayo kwa upande wake hajawahi kuitumia toka awe mteja wa benki hiyo.

Hata hivyo alisema baada ya kuhoji sana ndipo benki hiyo ilipoamua kuchunguza suala hilo na kubaini majina ya watu waliohamisha fedha hizo na kuwa hadi sasa suala hilo lipo polisi linafanyiwa kazi.Huku baadhi ya wateja wakienda benki hapo na polisi kutaka kufunga akanti zao na kuhama uteja na benki hiyo .Walidai kuwa kuna uwezekano wa wafanyakazi wa benki hiyo kukopeshana fedha zao kinyume na utaratibu na baada ya muda kuzirejesha.
Kwani walisema kuwa wakati mwingine baada ya kufika na kulalamika katika benki hiyo na kuambiwa wafiki baada ya siku mbili ama tano wmekuwa wakikuta akaunti zao zinapesa kama walivyoziacha .Mbunge wa jimbo hilo Filikunjombe amekili kupokea malalamiko hayo na kuwa tayari amewasiliana na meneja wa kanda na meneja wa benki hiyo ili kutolea ufafanuzi suala hilo.
Hata hivyo alisema kuwa majibu ambayo ameelezwa na viongozi hao wa kuwa yawezekana fedha hizo zinachnukuliwa na jamaa wa wateja hao ambao wamekuwa wakiwapa namba zao za siri bila kujua ama kwa kujua ama ni kampuni ya simu ambayo inashughulika na huduma hiyo .
Pia alisema kuwa ameshangazwa na ushirikiano mdogo wa wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Ludewa kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa wateja wao wenye matatizo hayo kwa kuwataka waende polisi kufikisha malalamiko yao huku wakijua wazi kuwa wateja hao wameingia mkataba na benki ya sio polisi .
Hata hivyo meneja wa NMB tawi la Ludewa alipotafutwa kwa simu alisema kuwa hana mamlaka ya kulizungumzia suala hilo na kuwa uongozi wa juu wa benki hiyo ndio unaweza kuzungumzia suala hilo . Du! Thanx 'Mzee wa Matukio' -Iringa.


2 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli nchi yetu inasikitisha sana,Ikiwa financial institutions kama benki zinakosa uaminifu sasa ni nani wa kuaminiwa ??? hapo ni uzembe au njama za hiyo benki na ingefaa uongozi mzima wa benki na wafanyakazi wao watoe maelezo yanayoeleweka kuhusu kashfa hii,yaani bongo watu hutafuta kila namna ya kujipatia pesa kwa haraka bila kujali risk zilizopo,jambo jingine linalochangia ni hizi huduma walizoanzisha za kutumiana pesa kwa kupitia simu zao za mikononi,hapo ndipo mianya ya wizi inapotokea na kwa vyo vyote benki lazima itakuwa inahusika.Itabidi watu warudi kuweka pesa zao mtungini au kuzifukia shambani,maana benki ndipo tunaamini kuna usalama wa pesa zetu sasa kama inakuwa hivi sijui tumuamini nani ???Uzembe na utapeli mkubwa huu.Mungu ibariki Tanzania yetu ya mateso !!!
Abbu Omar,Prof.Jnr Kanagawa-ken.

BM. said...

Kwa hakika prof. Abuu , mie nauhesabu huu kama uhujumu uchumi. Watu wakiacha kuweka pesa benki au wakikimbilia kwenye Benki za mataifa ya nje , benki za kizalendo zitafilisika. Nafikiria ingekuwa China au mataifa ya watu walio makini ingekuwaje. Kashfa hii ikithibitika inatosha kuwaondoa viongozi wa Benki hiyo hususan wenye vitengo vyao. lakini Bongo yetu ...mambo shwari tu inatisha!... Msulwa