Chama tawala nchini Japani cha Democratic kimemchagua Waziri wa fedha wa hapa Japani Yoshihiko Noda kuwa raisi wake, hali inayoonyesha ishara dhahiri kuwa muda mfupi ujao atashika nafasi ya Waziri Mkuu itakayoachwa na Waziri Mkuu wa sasa Naoto Kan abaye alijiondoa katika wadhifa huo ijumaa iliyopita.
(Naoto Kan Kulia- kushoto Yoshihiko Noda)Ilikuwa patashika kwa wagombea , katika uchaguzi uliofanyika leo Jumatatu, ambapo katika duru ya kwanza ya kujieleza na kupigiwa kura hakuna aliyetoka na ushindi wa mija kwa moja. Katika duru ya kwanza iliwashindanisha wagombea watano Waziri wa Uchumi Banri Kaieda na mh. Noda waliongoza na ikabidi wapigiwe tena kura ambapo Noda alipata kura 215 kati ya 395 huku mwenzake akiambulia kura 177.
Baraza la mawaziri litajiuzulu hivi karibuni na Bunge ndipo litakapomchagua Waziri Mkuu. kama ilivyotarajiwa aliwaambia waandishi wa habari mara tu baada ya kutangaziwa ushindi kuwa anataka kuzidisha kasi yabujenzi wa maeneo yaliyoathirika na tetemeko na tsunami , machi 11 mwaka huu.
Ni kawaida kwa Japani kubadilisha mara kwa viongozi wake wa juu na mabadiliko haya hayawashangazi sana Wajapani ...labda wageni kama akina siye!.Noda anakuwa waziri Mkuu wa Sita katika kipindi cha miaka mitano...
AFRIKA TUKUZE UCHUMI WA VYAMA VYAMA VYETU
3 hours ago
0 comments:
Post a Comment