Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, August 24, 2011

Mwanamke mmoja nchini Japani mwenye umri wa miaka 65 mwaka huu amejikuta akiiingizwa mjini baada ya kuhamisha mara kadhaa fedha bila kujua , ambapo alihamisha Yeni million 29 (sawa na Tsh. 580 Millioni) kwa mwanamume mmoja asiyefahamika ambaye amejifanya kuwa mwanawe wa kiume.
Polisi wameripoti jumamosi iliyopita kuwa utapeli wa aina hii unaofahamika hapa Japan kama ‘ “ore ore sagi,” ulihusisha mawasiliano kwa njia ya simu na mtu aliyekuwa akiamini kuwa ni mwanawe.Mtu huyo alimwambia huyo ‘mama yake’ kuwa amuhamishie fedha kwenye akaunti yake ili kulipa madeni yanayomkabili na ndipo alipoanza kumwaga pesa.Kulingana na ripoti iliyoonekana kwenye kituo cha televisheni cha Asahi, mama hyo anakaa maeneo ya Suginami na kwamba tukio hilo lilikuwa la June 17. Kwanza aliomba apelekewa Yeni laki sita na baada ya kumkubalia akawa anamuingizia fedha kwa zaidi ya mara 30 na zikafikia Millioni 29 kabla hajakutuka kuwa ameibiwa. Du!
Hii ilitokana na mama huyo kupokea simu ya mtoto wake wa ukweli wiki hii na baada ya kuripoti suala hilo Polisi , ikagundulika kuwa mtu huyo alikuwa akitumia akaunti tofauti za benki kwa kila hamisho moja la pesa.

1 comments:

Anonymous said...

Hiyo ni sawa kabisa maana hawa watu wamezidi roho mbaya na ubaguzi
inawezekana huyo mama alikuwa land lady,Tatizo la society hii ya wajapani ni ubinafsi na kuona nchi yao ndiyo heaven na ujinga huu hautakwisha maana kila siku wanaonywa na pia kwenye mabenki na Atm machines kuna matangazo ya kuwaonya,lakini ndiyo hivyo sikio la kufa halisikii dawa.Good news !!!mtoa maoni,tokyo.