Timu ya watafiti wa kijapani jana Jumatano ilibainisha uvumbuzi wao wa chombo ambacho wanasema kuwa kinaweza kupima kile kinachofanyika kwenye ubongo na kuweza kukitumia chombo hicho kuimarisha kazi za ubongo madarasani au katika pilikapilika za kimichezo.
Mainjinia kutoka kampuni ya elektroniki ya Hitachi waliofanya kazi bega kwa began a wanasayansi wanasema kifaa hicho chepesi kinachovaliwa kichwani kina uwezo wa kupima kwa usahihi mabadiliko yanayofanyika katika kipindi ha dakika moja tu cha kiwango cha damu katika ubongo , kitu ambacho ni muhimu sana kujua ni kwa kiwango gani kiungo cha mwili kinafanya kazi.
Vifaa kadhaa visivyounganishwa popote vinaweza kufanya kazi wakati huo huo huku taarifa za ubongo zikijionyesha kwenye skrini pale pale na kuwafanya watafiti kufuatilia kazi zinazofanyika katika ubongo kwa watu wanaofikia 20 kwa wakati mmoja.
Kampuni hiyo kubwa ya kijapani ya elektroniki imesema kuwa kwa sasa haina mpango ya kukifanya kifaa hicho kuwa cha kibiashara ambacho kwa kawaida hutumia mwanga wa mionzi kubaini kiwango cha damu katika ubongo.
MADAKTARI 120 WA WANYAMA WAFUTIWA USAJILI
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment