Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, September 30, 2011

Mke wa raisi wa Marekani Bi Michelle Obama jana aliwashangaza waliombaini baada ya jana alhamisi kuingia kwenye supermarket moja akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya kutokea, kofia inayovaliwa na wacheza baseball pamoja na miwani ya jua na kufanya manunuzi katika duka hilo linalofahamika kama Target Corp. store huko Alexandria, nje kidogo ya jiji la Washington.]...akiwa katika foleni ya kulipia vitu alivyonunua.

Timu ya walinzi ambayo haikujulikana na wateja waliokuwemo kwenye duka hilo kutokana na kuvalia nguo za kawaida walifika dukani hapo nusu saa kabla ambapo baadaye Bi obama aliingia katika duka hilo na kufanya manunuzi yake kwa dakika 40 , kisha akapanga foleni kwa keshia ili kulipia bidhaa zake.
Mtunza fedha alimgutukia baadaye alipoona jamaa mmoja akimpiga picha lakini vinginevyo zoezi hilo lingekwisha kimya kimya. Mwenyewe amichelle anasema kuwa anazikosa fursa hizo kutokana na wadhifa wake na kukaa katika white house.

Michelle anatajwa kuwa ni mke wa Raisi aliye wa kwanza kutoka nje kwa ajili ya manunuzi kwa mwonekano wa mwananchi wa kawaida ingawa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliwahi kuonekana mitaani na mume wake wakati wa mwisho wa wiki.

...(AP Photo]

0 comments: