Tetemeko kubwa lililofikia ukubwa wa 6.2 kipimo cha richa kimetikisa pwani ya Kaskazini Mashariki mwa Japani leoAlhamisi jioni , lakini hakuna hatari ya kutokea mawimbi ya tsunami kama ilivyotokea siku zilizopita. Hadi sasa hakuna taarifa za majeruhi wala uharibifu wowote uliotokea kutokana na mitetemo hiyo.
Shirika la Utabiri wa hali ya hewa limesema kuwa tetemeko hilo lilitokea saa kumi na moja jioni kwa saa za Japani (Afrika Mashariki saa tano asubuhi) kitovu chake kikiwa Pwani ya Ibaraki , takriban kilometa 220 Mashariki mwa jiji la Tokyo, kilometa 1o chini ya bahari.
Bado watu wa Japani wanakumbuka vyema vifo vya watu takriban elfu 20 au kupotea katika pwani hiyo hiyo ya kaskazini Mashariki kufuatia tetemeko na mawimbi makubwa ya tsunami , machi 11 mwaka huu .
Katika maafa hayo , Mtambo namba moja wa Nyuklia wa Fukushima uliharibiwa na zaidi ya watu laki moja walilazimika kuyahama makazi yao kwasababu ya tishio la kusambaa kwa mionzi ya Nyuklia.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Thursday, September 15, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment