Mwanamke mmoja nchini Japani mwenye umri wa miaka 45 anashikiliwa na Polisi kwa kumuuza binti yake kwa mteja mwanaume kwa akili ya ufanya naye mapenzi. Mwanaume huyo ana umri wa miaka 72 na ni mkazi wa eneo la Nagano hapa Japani.
Taarifa zilizotolewa na polisi zimebainisha kuwa mwanamke huyo alikuwa akimchukua binti yake huyo na kumpeleka kwenye Hoteli moja jijini humo ambako alipatiwa kitita chake na kumuacha binti yake hapo aendelee na mambo yao.Inaripotiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akipokea kati ya Yeni Elfu 20 na elfu 30 kila akifanya hivyo (Sawa na shilingi za Kitanzania kati ya laki nne na laki sita ).
Ingawa umri wa binti huyo haujawekwa wazi , msichana huyo anaaminika kuwa hajafika miaka 20 na zaidi na wakati alipokutana na mzee huyo alikuwa na miaka kumi na ushee hivi…
Inaaminika kuwa watu hao walikutana kwa miaka kadhaa wakiendelea na biashara yao iliyoonekana machoni mwa watu kama ‘Uhusiano wa kifamilia’, kumbe yalikuwa mengine!
Uhalifu huo uliwekwa wazi baada ya msichana mmoja anayesoma shule moja na binti huyo kutoa taarifa polisi akisema kuwa kulikuwa na jambo lilikuwa likiendelea baina ya watu hao.Polisi wamesema kuwa mwanamke huyo alikuwa akiendelea na biashara hiyo ya kumuuza mwanawe ‘kingono ‘kwa mzee huyo kwa miaka kadhaa. Uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, October 05, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment