Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, November 12, 2011

. Jioni ya leo nilifika katika hospitali iliyopo katika viunga vya jiji la Sagamihara, nchini Japani kumjulia hali Katibu Mkuu wa Umoja wa watanzania wanaoishi Japani-TANZANITE ambaye amelazwa hapo akipatiwa matibabu. Tuliongea kwa zaidi ya saa moja na nusu na anaeleza kuwa hali yake inazidi kuimarika na kwamba anatarajia hatua inayofuata ni kufanya mazoezi ya kitiba ili kuuweka mwili katika hali nzuri zaidi.Uchunguzi wa hospitali hiyo umeoyesha kuwa ajali hiyo aliyoipata ilitegua sehemu inayounga mguu wa kulia na nyonga na ameshafanyiwa upasuaji katikati ya mwezi uliopita wa oktoba ili kuziba mifupa iliyoachiana. Mwombeki aliniambia kuwa yuko kwenye hali nzuri sasa na ameacha kutumia dawa za kuondoa maumivu kwa muda kutokana na maumivu hayo kupungua ukali wake, kauli iliyoungwa mkono na mkewe anayemuuguza.Pole sana bro. Mwombeki Jr.

Nje ya hoospitali...

0 comments: