Leo nchini Japani ilikuwa siku ya mapumziko. Ilikuwa siku ya Utamaduni. Kuna historia ndefu ya sababu za maadhimisho ya siku hii.
Siku ya utamaduni ya Japani ilisherehekewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1948 kuadhimishwa kutangazwa kwa katiba mpya ya Japani baada ya vita vya pili vya dunia.
Hata hivyo siku hii ilishaanza kuwa siku ya kitaifa tangu mwaka 1868 na wakati huo ilikuwa ikiitwa TenchÅ-setsu, na ilikuwa ya kusherehekea kuzaliwa kwa mfalme wa tawala ya Meiji.Mfalme huyo alipokufa mwaka 1927 siku hiyo Novemba tatu ikabadilishwa na kupewa maana nyingine kuwa ni siku ya utamaduni.
Kwa wajapani hii ni siku takatifu sana. Wazazi hutoka na watoto wao kwa matembezi katika siku hii wakila na kunywa. Katika viunga vya Jengo la Utangazaji la Japani –NHK leo kulikuwa na maonyesho ya ngoma za utamaduni.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Thursday, November 03, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment