Kuanzia Feb mosi mwaka huu, matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani yatasikika moja kwa moja kupitia TBC FM Dar es salaam baada ya mkataba rasmi kutiwa saini mwishoni mwa wiki iliyopita Jumamosi tarehe 21/1...jijini Dar es salaam. Ilikuwa hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wa TBC Bw.Clement Mshana aliyetia saini kwa niaba ya TBC na Mwakilishi wa NHK World Bi Yuko Asano akiwa na ujumbe wake wa watu watano kutoka Japani.
Alikuwepo balozi wa Japani Nchini Tanzania Mh. Okada , Mkurugenzi wa habari maelezo Bw. Raphael Hokororo aliyesoma hotuba kwa niaba ya waziri wa Habari , utamaduni na Michezo mh. Emannuel Nchimbi,na wadau wengine wakiwemo wasikilizaji wetu waliotoka katika nchi za Kenya, Uganda na wa nyumbani Tanzania.Mwingine ni makamu wa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC na wafanyakazi wa TBC walitupa support sana..tafadhali fuatilia habari hizi kwa njia ya picha.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, January 24, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment