Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, February 05, 2012

Mashabiki wa mwanamuziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva nchini Tanzania Abasi Kisinza maarufu kjnl 20% ambaye wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha miaka saba au kulipa faini ya sh 200,000 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi mwaka jana bado wanaendelea kuumizwa na tukio hilo.
Mashabi hao wamesema kuwa mwanamuziki huyo amekuwa kama darasa la kimaisha kwao na hivyo kitendo cha kukutwa na hatia kimewasononesha. Wakiongea na Mirindimo kwa njia ya simu kutoka Dar kuhusu sakata hilo , mashabiki hao wamesema kuwa hilo liwe fundisho pia kwa wengine wenye tabia kama zao huku wakijua kuwa wana majukumu ya kijamii.
Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa gazeti la Habari Leo, Hakimu wa mahakama ya wilaya Kilwa mheshimiwa Arcado Chuwa alitoa hukumu hiyo baada ya kukamilisha kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, za utetezi na mashataka. Alisema ili kuwa fundisho kwa wengine baada ya mahakama kumtia hatiani anamhukumu kifungo cha miaka saba au faini ya sh 200,000.
Awali mwendesha mashitaka, wilayani Kilwa, Thomas alisema mtuhumiwa alikutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi gramu 20 mwaka jana mwezi wa Desemba wakati akiwa safarini kwenye kijiji cha Nangurukuru wilayani Kilwa akiwa katika gari lake.Hata hivyo 20 per cent alinusurika kutumikia kifungo kwa kulipa faini.

0 comments: