Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, October 09, 2008

(Picha na Issa Michuzi)
Mtanange wa sita wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 12 hadi 17 Februari 2009; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla ya machweo.
Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.
Likionyesha wasanii maarufu na wanaochipukia na waliofanyiwa uteuzi makini zaidi ya 400 (vikundi 40 kwa jumla), Sauti za Busara imeweza kuthibitisha kuwa ni tukio kubwa na bora zaidi la muziki hapa Afrika mashariki, ni tukio linalowaunganisha watu katika mazingira ya kusherehekea.
Tusikia fahari kutangaza kwamba Samba Mapangala amethibitisha kushiriki akiambatana na bendi yake ya Orchestre Virunga. Kwa hakika yeye ni mmoja wa wasanii mahiri na wanaopendwa sana hapa Afrika Mashariki. Katika muda wa miaka 25 ameweza kutamba na vibao mbalimbali, vikiwemo Virunga, Ahmed Sabit, Vunja Mifupa, Sungura, Vidonge, Dunia Tunapita na Nyama Choma.

Wasanii watakaoshiriki
Samba Mapangala & Orchestre Virunga (DRC/Kenya/USA), Msondo Ngoma Band (Tanzania), Omar Pene & le Super Diamono (Senegal), Mangala Camara (Mali), Nawal (Comoros/France), King Ayisoba (Ghana), TY (UK), Meta and the Cornerstones (Senegal/USA), The Moreira Project (South Africa), Comrade Fatso and Chabvondoka (Zimbabwe), Jagwa Music (Tanzania), AY (Tanzania), Joh Makini (Tanzania), Elemotho (Namibia), Segere Original (Tanzania), Best of WaPi (Pan Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar), Bi Kidude (Zanzibar), Iddi Achien'g (Kenya), Khethi with Kibo Sounds (South Africa/Tanzania), Rachel Magoola (Uganda), Wahapahapa Band (Tanzania), Omega Bugembe Okello (Uganda/USA), Aron Nitunga (Burundi/Canada), Safar (Zanzibar), Kiumbizi (Pemba), Zinduka Ngoma (Zanzibar), Dj Side (Zanzibar), and more to be announced

Kama ilivyo ada kutakuwa na matembezi ya ufunguzi wa tamasha siku ya tarehe 12 Februari, matembezi hayo yataambatana na burudani za Beni, Mwanandege, Ngongoti, wachezaji na wanasarakasi. Mkusanyiko huo utawasili maeneo ya Forodhani nyakati za saa kumi na moja alasiri na kuingia ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe.

Burudani kutoka Afrika chini ya anga
Kuanzia siku ya Alhamisi mpaka Jumapili, kutakuwa na burudani ya vikundi kumi kila siku. Wasanii wakubwa wataonyeshana kazi na wale wanaochipukia. Kwa pamoja tuna mseto wa vikundi thelathini kutoka Zanzibar, Tanzania bara na Afrika Mashariki. Vikundi hivi ni mchanganyiko wa vile vya muziki wa asili, vionjo mchanganyiko na ule wa kileo. Vilevile kuna vikundi vingine kumi kutoka Komoro, Zimbabwe, Afrika Kusini, Mali, Senegal, Ghana, Nigeria na Uingereza.Maonyesho yote huanza wakati wa jioni, muda ambao joto la jua linapoanza kungua, mara nyingi kundi la mwisho hupanda stejini nyakati za saa sita ya usiku.
Jukwaa kuu
Jukwaa kuu la burudani lipo eneo la Mji Mkongwe, ndani ya ukumbi wa kihistoria wa Ngome Kongwe (upande wenye majani) na juu upo wazi. Kipindi cha tamasha ukumbi huu hupambwa kwa rangi mbalimbali, na pia kunakuwa na karibu vibanda ishirini kwa ajili ya huduma za vinywaji, chakula, uuzaji wa nguo, bidhaa za kisanii, pamoja na kanda na CD za wanamuziki mbalimbali.
Pilika pilika ni nyingi kila siku ya tamasha ndani ya ukumbi huu, wenyeji na wageni wa rika, tamaduni na jinsia mbalimbali hujazana kwa wingi. Muda wa jioni kunakuwa na watoto na familia nyingi katika hali ya furaha na bashasha, wadau mbalimbali wa sanaa na utamaduni kutoka kona mbalimbali hubadilishana mawazo. Giza linapoingia wapenda muziki nao hujifaragua na kujirusha kutokana na mirindimo ya muziki na burudani mahiri.

Kila mtu anakubali kwamba kipindi nyoyo ya kila mhudhuriaji hukongwa kutokana na mandhari ya tamasha, na Sauti za Busara huthibitisha kuwa ni “tamasha rafiki zaidi duniani!”

Tiketi na viingilio
Kiingilio ni bure kila siku kuanzia saa kumi jioni hadi machweo. Baada ya hapo utahitajika kuwa na tiketi au pasi maalum ya kuingilia. Bei zinatofautiana baina ya wageni, wakaazi na. Kwa wanaopendelea kukaa kwenye viti kuna tiketi maalum za VIP.

Usafiri Na Malazi
Kwa mahitaji yako yote ya usafiri na malazi hapa Zanzibar pamoja na usafiri wa anga kwa Afrika, tunafurahi kukufahamisha kuwa wasiliana na Tabasam Tours iliyopo Zanzibar. Wao wanatoa huduma za uhakika za usafiri wa kwenda na kurudi uwanja wa ndege, maandalizi ya malazi na pia unaweza kupata pasi ya siku nne ya tamasha kupitia kwao.
Na zaidi ni kwamba kutakuwa na punguzo la asilimia 5 kwa wale watakaowatumia Tabasam Tours kufanya taratibu zao za malazi. Ulizia "Busara Discount".
Usafiri Na Malazi>>>

Sherehe ya kumalizia tamasha
Siku ya mwisho wafanyakazi wa tamasha, baadhi ya wasanii na wale wote wanaopenda kwa pamoja tutaelekea katika moja ya fukwe murua Zanzibar. Huko kutakuwa na ma-DJ, wacheza sarakasi, vikundi mbalimbali vya muziki na hivi ndivyo tutakavyohitimisha karamu yetu kwa mwaka 2009.
Shughuli hii imepangwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 17 Februari,

0 comments: