Tandale kwa mtogole....miundombinu jijini Dar es salaam. Bila shaka safari ni ndefu.
Ni hapa...
Mrembo wa Brazili aliyekuwa aiwakilishe Brazili kwenye Miss World ambaye alikatwa mguu na mkono ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa uliokuwa ukimkabili amefariki dunia.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alikuwa aiwakilishe Brazili kwenye mashindano ya urembo wa dunia, amefariki pamoja na kukatwa mkono na mguu ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa aliokuwa nao.Mariana Bridi da Costa alikatwa mkono na mguu katika jitihada za madaktari kuzuia kusambaa kwa bakteria waliotokana na maambukizi katika njia ya mkojo na kusababisha ugonjwa wa septicaemia.Madaktari walisema hali ya mrembo huyo ilizidi kuwa mbaya majira ya usiku na mrembo huyo alifariki asubuhi.Ugonjwa wake ulikuwa ukisababishwa na bakteria Pseudomonas aeruginosa ambaye anajulikana kuwa ni sugu kwa madawa mengi.Bridi alizidiwa mwezi wa disemba na kupelekwa hospitali ambapo madaktari walimwambia anasumbuliwa na mawe kwenye figo kabla ya kulazwa tarehe 3 mwezi huu katika hospitali moja kusini mashariki mwa Brazili.Rafiki wa kiume wa binti huyo, Thiago Simoes, alisema kuwa Bridi alizidiwa disemba 30 lakini madaktari walimwambia anasumbuliwa na mawe kwenye figo.Maambukizi yaliendelea kwenye mwili wake na kumsababishia kuzidiwa na kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi ndipo ukweli wa mambo ulipojulikana.Iliwabidi madaktari kukata mkono wake na mguu wake ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.Bridi aliwahi kufikia fainali mara mbili katika mashindano ya urembo kuwania mwakilishi wa Brazili kwenye Miss World.
Waziri mmoja mwanaume nchini Ufaransa amejitangaza kuwa yeye ni shoga na amemtaka Rais Sarkozy wa nchi hiyo amkubalie akitoa mualiko katika sherehe za serikali amualike yeye na mumewe, kwani yeye ni mchumba wa mtu.
Waziri wa Ufaransa anayehusika na ushirikianon wa bunge na serikali Roger Karoutchiunayeiona picha yake amejitokeza hadharani na kudai kwamba yeye ni shoga na ana mchumba wake wa kiume.Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa Karoutchi alisema “Ni kweli nina mchumba wangu ambaye ni mwanaume na nina furaha sana kuwa naye. Mimi ni shoga Naongea hivi kuweka wazi kwakuwa hamna haja ya kuficha " alisema waziri huyo.
Waziri huyo anayetegemea kutoa kitabu chake mwezi januari kitakachotoa siri zake nne amesema kuwa suala hili la kuwa shoga ameliezea vizuri katika kitabu chake hicho.Waziri huyo pia aliweka bayana kuwa ameishamjulisha rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kuwa yeye ni shoga na amemwomba akimwalika katika shughuli za kiserikali au binafsi amwalike aende na mwanaume wake kama mume wake.Shirika la habari la Ufaransa limesema kuwa katika siasa za Ufaransa waziri huyo amekuwa waziri wa kwanza kujitangaza kuwa ni shoga.Miaka 10 iliyopita Meya wa Paris Bertrand Delanoe wakati wa kampeni za uchaguzi alijulikana sana wakati huo alipojitangaza kuwa ni shoga.
Jamaa mmoja mkazi wa Gombolamboto Dar es salaam, amekutwa amekufa chumbani kwake baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka aliloninginiza katika dari la chumbani kwake baada ya kuambiwa na mchumba wake kuwa anatarajia kuolewa na mwanaume mwingine. Binti huyo anayemlalamikia anasemekana ni mzuri kupita kiasi . Aliyejinyonga alitambuliwa kwa jina la Joel Joel alikutwa akiwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka aliloninginiza katika dali la chumbani kwake.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu alikutwa kweli akiwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia shuka aliloning’iniza kwenye dali chumbani kwake.Alisema chanzo cha kifo kilijulikana baada ya marehemu kuacha ujumbe kuwa amejiua kutokana na kusalitiwa na mpenzi wake wa siku nyingi aliyekuwa anampenda na alikuwa anatarajia kufunga nae ndoa mwaka huu.Ujumbe ulisema kuwa “Nimejinyonga kutokana na mchumba wangu ambaye nilitarajia kufunga nae ndoa kuniambia kuwa anatarajia kuolewa na mwanaume mwingine”“Tulishaahidiana kuoana mwaka huu na wazazi wa pande zote mbili walishabariki kwa matarajio yetu, najinyonga kutokana na aibu kubwa niliyoipata kwa ndugu na jamaa zanguNitaiweka wapi sura yangu tulipendana nae sana lakini ameamua kunisaliti, najinyonga kwa kuwa awali nilichaguliwa mchumba na wazazi niliwaambia nina mchumba wangu ninayempenda ambaye leo hii amenidhalilisha hivi” ByeBye ulimalizia ujumbe huo. Kifo cha mapenzi..
Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe amempa kipondo mpiga picha toka Uingereza alipojaribu kumpiga picha ya karibu wakati mke huyo wa rais alipokuwa likizo nchini Hong Kong kumtembelea binti yake.
Mpiga picha huyo toka Uingereza amelalamika kuwa mke wa rais wa Zimbwabwe alimpiga magumi ya uso mara kibao alipojaribu kumpiga picha karibu na hoteli moja ya kifahari jijini Hong Kong.Richard Jones aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Grace Mugabe, 43, aliwaamuru walinzi wake wamkamate mpiga picha huyo na kumshika kwa nguvu wakati mke huyo wa rais alipokuwa akitoa kipondo kwa mpiga picha huyo."Alinitandika ngumi kadhaa usoni" alisema Jones. "Alikuwa amevaa pete ya almasi ambayo ilinisababishia majeraha kadhaa usoni".Jones, 42, kutoka Machen kusini mwa Wales, alikuwa Hong Kong kwaajili ya gazeti la The Sunday Times lenye makazi yake London, Uingereza.Jones alisema kuwa ngozi ya uso wake ilipata mipasuko zaidi ya 10 ingawa hakuhitaji kupelekwa hospitali.Msemaji wa polisi wa Hong Kong Odelia Tam alisema kuwa polisi wanachunguza mkasa huo na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa.Ubalozi wa Zimbwabwe Beijing ulikataa kujibu simu zote zilizokuwa zikitaka ufafanuzi wa suala hilo.Mke huyo wa rais wa Zimbwabwe alikuwa Hong Kong kumtembelea binti yake Bona anayesoma nchini humo.Inasemekana Grace Mugabe aliondoka Hong Kong baada ya mkasa huo wa kumpa kisago mpiga picha huyo.
Anga ya jiji la Ukanda wa Gaza lilifunikwa na vikaratasi vilivyomwagwa na majeshi ya Israel kuwataka watu walio na habari walipo wapiganaji wa HAMAS watoe taarifa.
Inaingia wiki ya tatu ya mashambulizi Wapalestina 1,015 wamekwisha uwawa na waisrael wanne.Fuatilia kadhia hiyo katika picha kutoka mashirika ya kimataifa.