Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, February 17, 2009

Muimbaji mwenye sauti tamu wa Baba ya Muziki Msondo Ngoma Joseph Maina amefariki leo asubuhi akiwa kwenye daladala eneo la Temeke la Mikoroshoni, Dar akielekea studio za Osterbay kufanya Recording. Ni pigo kwa wapenda muziki wa dansi, wapenzi wa Msondo na wasanii kwa ujumla. Bendi hiyo imekwishaondokewa na wanamuziki watatu wengine wa safu ya mbele na kubakisha kilio kikubwa. Waliofariki ni pamoja na Tx Moshi William, Suleiman Mbwebwe na Momba (baba Natasha). Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Kiongozi wa Bendi hiyo Muhidini Gurumo. Mungu ailaze roho yake peponi Amin.

0 comments: