Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, March 23, 2009

Akielezea kifo cha binti yake, mama yake mrehemu aitwaye Jackiey Budden mwenye umri wa miaka 50 sasa alielezea jinsi alivyoung'ang'ania mkono wa binti yake wakati alipokuwa kwenye dakika za mwisho mwisho za kukata roho.Jade alifariki jana asubuhi akiwa nyumbani kwake kwenye kitongoji cha Upshire, Essex, nchini Uingereza akiwa amezungukwa na ndugu zake wa karibu na marafiki zake.
Hebu soma historia yake hapa; Jade alizaliwa mwaka 1981 na alijipatia umaarufu nchini Uingereza baada ya kushiriki mashindano ya Big Brother mwaka 2002 na tangia hapo alikuwa hakosekani kwenye udaku kwa vimbwanga vyake mbali mbali kikiwemo kile kilichotokea mwaka 2007 wakati aliposhiriki mashindano ya Big Brother ya watu maarufu duniani na kulaumiwa kwa ubaguzi aliomfanyia mwanadada Shilpa Shetty wa India.Jade aligundulika ana kansa wakati alipokuwa akishiriki mashindano ya Big Brother ya India mwaka 2008.Jade alirudi Uingereza kuanza matibabu na miezi miwili iliyopita madaktari wake walimwambia atafariki ndani ya wiki chache kwa kuwa kansa yake ilikuwa imeishaenea mwili mzima.Jade aliamua kufunga ndoa na mpenzi wake Jack Tweed wiki mbili baada ya kupewa taarifa hiyo na baadae aliamua kubatizwa yeye na watoto wake akiwa hospitalini hajiwezi.Kabla hajafariki Jade inasemekana alikuwa ameishapangilia mazishi yake yatakavyokuwa akitaka mazishi yake yawe kama sherehe kubwa ya kuwaaga watu kwa mara ya mwisho.Msemaji wake Max Clifford alisema kuwa Jade anataka jeneza lake lisindikizwe na msururu wa magari yatakayokatiza mitaa ya Esex alikokulia.Jade pia alitaka sala za mazishi yake zionyeshwe live kwenye televisheni kubwa zitakazowekwa nje ya kanisa atakalopelekwa.Inasemekana pia Jade pia alishagua nyimbo za kusindikiza jeneza lake.Kifo chake kimewahuzunisha wengi akiwemo waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown aliyeelezea kusikitishwa sana na kifo chake.Kifo chake kinasemekana kitaokoa maisha ya wanawake wengi kutokana na kuongezeka kwa jitihada za kupambana na Cervical Cancer iliyosababisha kifo chake.Mamia ya watu wameendelea kumiminika nyumbani kwa mama yake kuweka maua na kutoa salamu zao za pole.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu Jade peponi , Amin.

0 comments: