Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, March 23, 2009

Hatimaye yule nyota wa Televisheni Jade Goody, aliyekuwa akikisubiri kifo kwa siku kadhaa baada ya madaktari kumwambia ajiandae kufa kutokana na na kufikia kiwango cha kutisha cha Kansa. Amefariki dunia jana Jumapili akiwa na miaka 27. Kilikuwa kifo kichungu na alijiandaa kwa ushujaa mkubwa wa kibinaadamu kwa kufunga ndoa ya kidini katika siku zake za mwisho. Mambo mengine ni kuandaa mazishi yake mwenyewe na kuingia mkataba na shirika moja la Tv kutangaza mazishi yake.
Waziri Mkuu wa Uingereza wa Uingereza anaongoza shughuli ya maombolezi.Kifo kilimkuta wakati akiwa usingizini huku amezungukwa na mume wake Jack Tweed na mama yake Jackiey Budden .Ameondoka duniani na kuwaacha watoto wake wawali wadogo wa kiume. Mazishi yatafanyika baada ya siku 10 na mwili wake umeshapelekwa nyumbani kwake.

0 comments: