Nyota wa vipindi vya televisheni Uingereza, Jade Goody ambaye kwa mujibu wa madaktari wake, siku zake za kuishi duniani zimekaribia ukingoni ameanza kuwaaga ndugu zake na kupangilia taratibu za mazishi yake ambayo anataka yawe kama sherehe.
Jade ameanza kuwaaga rafiki na ndugu zake huku akipangilia mazishi yake ambayo yamepangwa kurushwa live kwenye luninga kubwa zitakazowekwa nje ya kanisa ambalo sala za maombi kabla ya mazishi zitafanyika.Jade ambaye anasumbuliwa na kansa alizidiwa mwishoni mwa wiki na hali yake imekuwa mbaya sana kiasi cha kwamba inasemekana ana ongea kwa tabu sana huku karibu masaa yote yakipita akiwa usingizini.Rafiki yake ambaye pia ndiye msemaji wake Max Clifford alisema kuwa Jade ameishaandaa mipangilio ya mazishi yake ambayo anatarajia yawe kama "sherehe" ya maisha yake."Anataka mazishi yake yawe kama sherehe kubwa sana kwakuwa ndio atakuwa akiwaaga watu wote kwa mara ya mwisho" alisema Clifford."Itakuwa ni siku ya Jade Goody, itakuwa kama anavyotaka iwe".Mazishi yake yatasindikizwa na msururu wa magari utakaopita kwenye mitaa ya kusini mwa London alikokulia.Inasemekana pia kuwa Jade ameishagua mpaka nyimbo za kusindikiza jeneza lake mojawapo ikiwemo nyimbo " All Things Bright and Beautiful".Jade aliwaambia watoto wake wenye umri wa minne na mwingine mitano wanaoishi na baba yake kuwa muda si mrefu atapaa kwenda peponi."Nitakuwa mojawapo ya nyota angani, kwahiyo mkiangalia angani mtakuwa mkiniona, siku zote nitakuwa nikiwaangalia" alisema Jade alipokuwa akiongea na wanae."Mama anatakuwa juu akiwaangalia, fungeni macho yenu na mtaweza kuongea nami"."Anazidi kudhoofika kila siku, tupo kwenye njia panda, hakuna mtu anayejua wakati gani atafariki kama ni baada ya dakika tano au siku tano" alisema msemaji wake huyo."Hata hivyo yuko pamoja na watu aliotaka awe nao pamoja katika masaa yake ya mwisho mwisho" alimalizia kusema msemaji wake huyo.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, March 17, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment