Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, March 26, 2009

Ajali za barabarani zipo nchi Japani ingawa si nyingi sana mwaka uliopita wa 2008 ajali 760,000 zilitokea nchini Japani, taifa lenye watu takriban millioni 130. Watu waliopoteza maisha walikuwa 5,155. Jamaa wakali sana hapa kwa madereva walevi. Ukikutwa umekunywa hata nusu glasi tu ya pombe na unaendesha gari kifungo kisichozidi miaka mitano jela ama faini isiyozidi Shillingi za kitanzania Millioni 14 hivi na ukipanda gari linaloendeshwa na mtu aliyekunywa pombe jela miaka mitatu au faini millioni saba hivi za kitanzania kwakuwa umeshabikia kutendwa kwa kosa hilo upo hapo!

0 comments: