Sizakele Khumalo...Mke mdogo wa Jacob Zuma huenda akawa First lady...Hatihati hii inakujaje..Hebu mwangalie Jacob Zuma mwenyewe...
Zuma ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 67 ni dhahiri atatangazwa rais mpya wa Afrika Kusini kutokana na matokeo ya awali ya uchaguzi wa Afrika Kusini yanavyoonyesha.Mjadala upo kwenye kujua je Zuma atamchagua mke wake yupi kuwa mke wa kwanza wa rais First Lady wa Afrika Kusini au kama atamchagua binti yake ambaye yuko naye kila kona kuwa First Lady wa Afrika Kusini."Nawapenda wake zangu na najivunia watoto wangu" ndilo jibu analolitoa Jacob Zuma anapoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na mjadala huu.
Taarifa zinasema kwamba Zuma ameoa wake sita na mke wake wa mwisho alimuoa mwezi january na idadi ya watoto wa Zuma inakisiwa kuwa kati ya watoto 13 na 22.Kutokana na Zuma kujulikana kama mpenda "dogo dogo" kuna uwezekano wa Zuma kuwa na wake wengine na watoto wengi ambao hawatambuliki rasmi.Zuma ambaye alitumia maisha yake ya mwanzoni kama mfugaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika Zululand, anafaidika na mabadiliko ya sheria nchini Afrika Kusini ya mwaka 1998 ambayo yaliruhusu na kuzitambua ndoa za kijadi na ndoa za wake wengi.Zuma alishatamba awali kuwa yeye yuko wazi kwenye masuala ya ndoa sio kama viongozi wengine duniani ambao huwa na wake wengine kwa siri.
Ni wake wanne wa mzee Zuma wanaotambulika kisheria, mmojawapo alikuwa Kate Mantsho Zuma ambaye alijiua mwenyewe mwaka 2000. Mke mwingine wa Zuma alikuwa Nkosazana Dlamini Zuma ambaye ndoa yao ilivunjika lakini wamekuwa karibu sana kutokana na kwamba bi Dlamini ndiye waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini kwa sasa na inasemekana Zuma anaweza akamuacha aendelee na wadhifa wake huo.Nompumelelo Ntuli, 34, aliyefunga ndoa na Zuma mwaka jana na anayeishi katika nyumba yake ya asili mjini Zululand inasemekana kuwa ndiye atakayekuwa chaguo la Zuma kuwa First Lady wa Afrika Kusini.
Mke wa kwanza wa Zuma aliyefunga naye ndoa mwaka 1973 Sizakele Khumalo, hapewi nafasi kubwa ya kuwa First Lady pamoja na Zuma kumuelezea kama mke wake mpendwa anayemuona pia kama dada yake katika harakati za ukombozi.
Binti wa Zuma, Duduzile anaweza akanyakua majukumu ya First Lady kirahisi kutokana na kwamba muda wote yuko bega kwa bega na baba yake na anahesabika kama mdau mkubwa wa karibu wa Zuma.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, April 25, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment