Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, April 25, 2009


Bi. Bette Calman Kwa miaka 40 amekuwa akifundisha Yoga na sasa ndio kwanza anajaribu kufanya mazoezi magumu zaidi. Bi Calman anapiga pushap bila matatizo, ana uwezo wa kujinyanyua vyuma na kukaa kichwa chini miguu juu huku mikono yake ikibeba uzito wa mwili wake wote pamoja na mazoezi mengine ambayo huwatoa jasho hata vijana wa miaka ya 20. Pia ana uwezo wa kupitisha kichwa chake kwenye magoti na kujinyanyua kwa kutumia mikono yake. Bi Calman alitamba sana nchini Australia kwenye miaka ya 1950 akiendesha vituo vya Yoga kwa miaka 33 na alikuwa na vipindi kwenye luninga kwenye miaka ya 1970.
Haya mzawa nawe anza kupiga samasoti…usisingizie umri lakini pembeni uwe umeweka dawa ya kuchua tu..haya anza.

0 comments: