Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, April 18, 2009

Watoto walio tumboni wataanza kusikilizishwa muziki wakiwa tumboni baada ya mp3 player kwaajili ya wototo walio tumboni inayoitwa 'Blaby' kuvumbuliwa na wagunduzi wake wamedai itawafanya watoto wawe 'maGenius' watakapozaliwa
Wanawake wajawazito wamepatiwa silaha mpya itakayowageuza watoto wao kuwa wenye akili sana "Genius". Silaha hiyo mpya ni Mp3 Player ya watoto ya "Baby Ipod" ambayo wagunduzi wake wanadai itawasaidia akina mama wajawazito kuwapa burudani watoto wao walio tumboni."Baby Ipod" hiyo imepewa jina la "Blaby" na ipo kwenye mkanda ambao huzungushiwa tumboni ikiwa na spika tatu zenye kutoa mtikisiko muziki unapochezwa. Wazazi wanaweza kuweka muziki yao kwenye hiyo Blaby au kurekodi sauti zao na kuwaikilizisha watoto wao walio tumboni.Mgunduzi wa kifaa hicho Geof Ramsay, raia wa Kanada alisema kwamba kifaa hicho kinatumia faida ya maelezo ya kisayansi yanayosema "Watoto hupata uelewa zaidi kama watasikilizishwa muziki wa Classic wakati wa ujauzito"."Wanasayansi wamezungumzia kwa miaka mingi sasa kwamba muziki unachangia kuongezeka kwa haraka kwa ufahamu wa mtoto" alisema Ramsay.Ingawa watoto hawawezi kusikia sauti kutokana na kimiminika cha amniotic kinachowazunguka wakiwa tumboni, wanaweza wakasikia sauti kutokana na mawimbi ya sauti yatakayotoka kwenye mtikisiko unaotolewa na spika za Blaby.Kifaa hiki kitasaidia akina mama kuthibitisha maelezo hayo ya kisayansi na kukuza uhusiano wao na mtoto aliye tumboni."Ni kweli kwamba muziki wa Classic ndio ambao uliopendekezwa na wataalamu lakini huwezi kuwazuia watu kuwapigia watoto wao nyimbo wanazozipenda", alisema Ramsay.

0 comments: