Stress ,kisayansi ninini!.....Sasa pata undani wa stress kwa kutumia uchambuzi huu wa kisayansi. Kwa hakika stress ni mkandamizo wa mawazo unaotokana na sababu mbalimbali.Pale unapopata tishio lolote lile mivumo yako ya ufahamu ya neva hujibu haraka kwa kutoa kitu kinachoitwa homoni za stress- stress hormones ambazo zina mchanganyiko wa adrenaline and cortisol. Homoni hizi zinauamsha mwili kwa hatua za hatari . Kuanzia hapo moyo wako utadunda sana, misuli itabana na kunakuwa na msisimko wa kutosha wa mwili. Mabadiliko haya yanakuongezea nguvu fulani na kukupa ujasiri wa kufanya maamuzi ya kujihami kwa haraka sana. Na ndipo hapo unajikuta ukikuta kitu cha kutisha unasimama ghafla na nywele zinakusimama. Kwa lugha nyepesi aina hii ya stress inajenga mazingira ya kukusaidia . Msaada huu una kikomo chake . Stress ikipita mstari Fulani inaanza kuleta madhara makubwa ya kiafya . Inavuruga furaha yako , mahusiano na hata kukusababishia magonjwa makubwa. Hivi unajua unaweza kupata kisukari , na hata kupunguza kinga ya mwili kwa kuwa na stress? Kwani unaweza kuidhiti vipi! Sasa soma Mirindimo ya Jumamosi kesho katika blog hii ujiepusha na balaa la stress sugu inayoweza kubadili rangi ya maisha yako!..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment