MTANZANIA Ahmed Khalfan Ghailani, anayetuhumiwa kushiriki katika tukio la ugaidi la kulipua ofisi za ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya, ametolewa katika gereza la Guantanamo Bay, nchini Cuba na kusomewa mashtaka katika mahakama ya shirikisho iliyoko Manhattan iliyoko New York. Ulipuaji wa ofisi hizo unaodaiwa kupangwa na mtandao wa kigaidi wa al Qaeda unaoongozwa na Osama bin Laden, ulifanyika siku moja na kwa muda unaolingana Agosti 7, 1998.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Sheria ya Marekani, Ghailani ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza kusomewa mashtaka hayo, alifikishwa katika Kituo cha Kurekebisha tabia kilichoko New York na kisha kupelekwa mahakamani kusomewa tuhuma zinazomkabili.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Eric Holder alieleza kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema kuwa Kufikishwa kwake katika mahakama ya shirikisho, Ahmed Ghailani anawajibika kwa tuhuma dhidi yake kuhusu ulipuaji wa Balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya na kusababisha vifo vya watu 224,
Ghailani anakabiliwa na mashtaka 286 ikiwemo kushirikiana na Osama bin Laden na wanachama wengine wa al-Qaeda kufanya mipango ya kuwaua Wamarekani popote walipo duniani, pia mashtaka ya mauaji kwa kila mtu aliyeuawa katika milipuko hiyo jijini Dar es Salaam na Nairobi Agosti 7, 1998.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, June 12, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment